Ripoti ya Taasisi ya Haki za
Binadamu imesema wagonjwa wa akili wanawake nchini India hufungiwa
kwenye taasisi za wagonjwa hao wakidhalilishwa kingono na kufanyiwa
ukatili, huku wakiishi kama wanyama.
Wanawake hao huwekwa kwenye taasisi
za wagonjwa wenye akili za umma zenye mrundikano, zisizo na huduma za
msingi, ambapo wagonjwa wa akili na walemavu nchini India huogopwa,
hutengwa na kunyanyapaliwa.
Ripoti hiyo ya Human Rights Watch
imesema wanawake na wasichana wenye ulemavu nchini India,
wanakabiliwa na changamoto zikiwemo za ukatili wa kingono pamoja na kuzuiliwa
kupata huduma za afya ya uzazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni