Imebainika kuwa ndege binafsi
aliyopiga nayo picha mwanamuziki Justin Bieber, hakuinunua bali
ilitolewa kwa ajili ya msanii huyo kutanua nayo wakati wa sikukuu
akitokea Canada kuja New York, na ukweli ni kwamba ndege hiyo ipo
sokoni.
Msanii Justin Bieber ambaye
inaaminika anamali za thamani ya dola milioni 200, itakuwa ni hatari
kwake kuinunua ndege hiyo yenye thamani ya dola milioni 60 ikiwa
mpya.
Siku ya Alhamisi, mpenzi wake ambaye
wamekuwa wakiachana na kurudiana Selena Gomez alijipiga picha akiwa
ndani ya ndege hiyo nzuri yenye viti 20 vya abiria, na kisha kutuma
kwenye mitandao ya jamii.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni