.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Desemba 2014

MTUMISHI WA AFYA ALIYEREJEA SCOTLAND KUTOKA AFRIKA ABAINIKA KUWA NA EBOLA

Mtumishi wa afya ambaye amerejea kutoka Afrika Magharibi, amebainika kuwa na virusi vya Ebola, na anapatiwa matibabu katika hospitali Jijini Gasgow.

Mwanamke huyo aliyewasili akitokea Sierra Leone usiku wa jumapili, amewekwa kwenye chumba cha pekee kwenye hospitali ya Gartnavel.

Watu wote waliokutana na mtumishi huyo wanachunguzwa, wakiwemo walikuwa nae kwenye ndege kuja Scotland hadi Heathrow.

Waziri wa Afya wa Uingereza, Jeremy Hunt amethibitisha kuwa mtumishi huyo mwanamke atapelekwa katika kitengo maalum Jijini London.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni