Maafisa nchini Indonesia wanatuma
timu kuchunguza taarifa za kuonekana kwa moshi kwenye eneo la kisiwa
ambalo ndege ya AirAsia namba QZ8501 ilitoweka.
Zoezi la ushirikiano la msako wa
ndege hiyo limeingia siku ya tatu, huku eneo msako likitanuliwa na
kufikia zoni 13 katika ardhi na baharini.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,
ikiwa na watu 162 ikitokea Surabaya, Indonesia kwenda Singapore,
ilitoweka siku ya jumapili.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni