.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Januari 2015

AFCON 2015 PAMOJA NA KUFUNGANA BAO 1-1,TUNISIA NA CONGO ZASONGA MBELE HATUA YA ROBO FAINALI

Tunisia na Congo zimefanikiwa kusonga mbele katika fainali za kuwania kombe la Mataifa Afrika, fainali zinazoendelea kuunguruma nchini Equatorial Guinea. 

Katika mchezo huo wa kundi B uliokuwa wa kukamilisha ratiba, timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa zimefungana bao 1-1.
Tunisia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa katika dakika ya 31 na Ahmed Akaichi, bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili Congo walijibu mashambulizi na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 66 mfungaji akiwa ni Bokila.
Kwa matokeo hayo, Tunisia imemaliza wakiwa vinara wa kundi B kwa kuwa na pointi 5 wakifuatiwa na Congo wenye pointi 3. Zote zimesonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni