.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 3 Januari 2015

BALOZI SEIF AZITAKA FAMILIA ZINAZOISHI KATIKA NYUMBA ZILIZOCHAKAA KUONDOKA MARA MOJA KUNUSU MAISHA YAO

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia nyumba iliyoporomoka dari na kujeruhi wakazi wake watatu hapo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Mzee Abdulla Juma.
Balozi Seif akiwaagiza watu wanaoishi ndani ya nyumba iliyoporomoka dari Mtaa wa Ukutani kuhama ili kunusuru maisha yao kutokana na uchakavu wa nyumba hiyo. Aliyepo mwanzo kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mmiliki wa nyumba iliyoporomoka Dari eneo la Ukutani Bwana Mzee Abdulla Juma na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee wakiangalia hali halisi ya mazingira ya nyumba hiyo.
                                                                 
                                                             Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza wananchi wanaoishi kwenye nyumba mbovu na zile zilizochakaa ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar wafanye utaratibu wa kuhama kwenye nyumba hizo mapema iwezekanavyo ili kunusuru maisha yao.

Alisema Serikali kamwe haitakuywa tayari kuachia wananchi wake wanaendelea kuishi katika mazingira ya hatari wakati njia za kuepuka hatari hizo zipo na wala hazina gharama yoyote.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua Nyumba ya Bwana Mzee Abdulla Juma ambayo iliporomoka dari sehemu ya sebule na kujeruhi wakaazi watatu wa nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Ukutani Mjini Zanzibar.

Watu waliojeruhiwa ni wadogo wa Mmiliki wa Nyumba Hiyo Bwana Haroun Abdulla Juma na Fahim Abdulla Juma waliolazwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu pamoja na Peter Monga aliyetibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni