Makumi ya watu wameuwawa ama
kujeruhiwa katika mlipuko nje ya chuo cha polisi katika jiji la Sanaa
nchini Yemen.
Taarifa zimeeleza kuwa bomu hilo
lilikuwa kwenye gari lililipuliwa karibu na kundi la wanachuo, hata
hivyo taarifa hizi bado hazijathibitishwa na mamlaka za nchi hiyo.
Mashahidi wamesema mlipuko huo
uliweza kusikika katika eneo kubwa la Jiji la Sanaa, na moshi mkubwa
umekuwa ukionekana.
Nchi ya Yemen imeendelea kuwa
haijatulia tangu kuibuka maandamano mwaka 2011, yaliyomlazimisha rais
aliyekuwa madarakani wakati huo Ali Abdallah Saleh kuachia madaraka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni