Sehemu ya nyuma ya ndege iliyoanguka
ya AirAsia namba QZ8501 imepatikana katika bahari ya Java, mkuu wa
zoezi la kutafuta ndege hiyo ameeleza.
Sehemu hiyo ya ndege ndiyo inayokaa
kisanduku cha kurekodi sauti na data itawasaidia wachunguzi kubaini
nini haswa chanzo cha ajali hiyo.
Ndege hiyo aina ya Airbus ilitoweka
katika rada wakati ikitokea Surabaya, Indonesia kwenda Singapore
Desemba 28, ikiwa na watu 162. Hakuna mtu aliyenusurika
aliyepatikana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni