.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Januari 2015

MMOJA WA KAMANDA MWANDAMIZI WA WAASI WA LRA AJISALIMISHA KWA VIKOSI VYA MAREKANI

Mtu anayedai kuwa ni kamanda mwandamizi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) anashikiliwa na vikosi vya Marekani.

Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dominic Ongwen, amejisalimisha katika nchi ya Afrika ya Kati (CAR) Idara ya Marekani imeeleza.

Ongwen anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, kwa kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Ongwen anachukuliwa kama naibu kamanda wa kundi hilo la LRA, ambalo kiongozi wake ni Joseph Kony.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni