.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 2 Januari 2015

COASTAL UNION YAANZA KUZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT RUVU HAPO KESHO

TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.

Akizungumza leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa
Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza
kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari Kocha wao mkuu Mkenya James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.

Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari,Kocha Mkuu
wa timu hiyo,Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na
kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi
kwenye mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni