.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 3 Januari 2015

KILIMANJARO FC YAITAMBIA HAI CITY

KOCHA wa Klabu ya Kilimanjaro FC ya mjini Moshi, Ally Chandika, amesema atahahakikisha timu yake inavuna pointi muhimu kutoka kwa vinara wa ligi daraja la Tatu, hatua ya sita bora, klabu ya Hai city ya wilayani Hai, katika mchezo wa kumalizia mzunguko wa kwanza, utakaopigwa kesho (Jumapili), kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, mara baada ya mazoezi
ya klabu hiyo yanayofanyika katika uwanja wa Mandela-Pasua, Chandika
amesema pamoja na changamoto zilizopo klabuni hapo vijana wake wako tayari kwa mchezo wa kesho hali inayochagizwa na ushindi wa 4-1 walioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Kilimanjaro.

Amesema pamoja na ugumu wa mchezo dhidi ya Hai city, ana uhakika wa
kuondoka uwanjani na pointi tatu muhimu na kwamba tayari wachezaji
wake ameshawaanda kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kutambua umuhimu wa
kushinda mchezo huo kwa lengo la kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea
mzunguko wa pili.


Kilimanjaro FC hadi sasa iko katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi zake saba baada ya kushuka dimbani mara huku Hai City wao
wakijivunia kushika usukani wa msimamo wakiwa na pointi zao tisa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni