Nchi ya Liberia imeondoa amri ya
kutotembea ovyo na mikusanyiko iliyowekwa kukabiliana na Ebola, ili
kuwaruhusu waumini kwenda makanisani kuhudhuria ibada ya mwaka mpya.
Hata hivyo Wizara ya habari
imewatahadharisha waumini kutorundikana na kusongana ama kushikana
mikono, ili kuzuia kuusambaza ugonjwa huo hatari.
Serikali ya Liberia ilikuwa
inatarajia kutokuwa na Ebola wakati wa Krismasi, hata hivyo ugonjwa
huo umekuwa ukiendelea kuchukua maisha ya watu nchini humo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni