.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 1 Januari 2015

WATU 36 WAFA BAADA YA KUKANYAGANA USIKU WA MWAKA MPYA NCHINI CHINA

Maafisa wa serikali ya China wamesema tukio la watu kukanyanga katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya Jijini Shanghai limeua watu 36, na kujeruhi wengine 47.

Kukanyagana huko kumetokea katika eneo la Chenyi square Jijini Shangahia ambapo maelfu ya watu walikusanyika kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya.

Mitandao ya jamii, imeeleza kuwa tukio hilo la watu kukanyagana lilichochewa na kitendo cha watu waliosimama kuchukua fedha feki zilizokuwa zikirushwa kwenye eneo la kibaraza cha juu cha klabu ya usiku.
                            Furaha ya Mwaka Mpya ikageuka kuwa ni vilio na majonzi 
                             Waombolezaji wakiweka maua katika eneo la Chenyi Square

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni