.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 10 Januari 2015

LIGI KUU UINGEREZA KUENDELEA LEO, CHELSEA, MAN CITY NA LIVERPOOL ZOTE KUSHUKA VIWANJANI

Ligi kuu nchini Uingereza kuendelea leo katika viwanja mbalimbali, ambapo vinara wa ligi hiyo matajiri wa London, Chelsea watakuwa nyumbani kucheza na Newcastle. 

Mchezo huo ni muhimu sana kwa Chelsea, kwani kama wakifungwa au kulazimishwa sare, halafu mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City wakaibuka na ushindi dhidi ya Everton katika mchezo mwingine wa ligi kuu utakaochezwa leo, basi Chelsea watakuwa wameondolewa kileleni. 

Chelsea na Man City wana pointi 46 kila mmoja, idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa sawa, hivyo yeyote atakayeteleza leo atakuwa amempisha mwenzake nafasi ya kuongoza ligi. 

Michezo mingine itakayochezwa leo ni kama ifuatavyo:-

Sunderland vs Liverpool

Burnley vs QPR

Leicester vs Aston Villa

Swansea vs West Ham

West Brom vs Hull

Crystal Palace vs Tottenham

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni