Wachezaji nyota Lionel Messi na
Neymar wamerejea kwa kishindo na kumaliza dhahama za vipigo kwa
kuiongoza Barcelona kuichakaza Elche kwa mabao 5-0 katika kombe la
Copa del Rey.
Wawili hao walipumzishwa jumapili na
kujikuta Barcelona ikipoteza dhidi ya vijana wa kocha David Moyes,
Real Sociedad, lakina jana usiku Neymar alikuwa wa kwanza kucheka na
nyavu baada ya kupata pande kutoka kwa Luis Suarez.
Katika mchezo huo, Suarez alifunga
bao la pili dakika 40 na Messi kuongeza la tatu katika dakika ya 45,
Alba naye akafunga dakika ya 56 na Neymar tena akacheka na nyavu
dakika ya 59 na kukamilisha karamu ya magoli.
Neymar akimchambua kipa wa Elche
Suarez akijipinda kufunga bao
Lionel Messi akifunga kwa shuti la penati




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni