Timu inayotafuta ndege ya Indonesia
inaamini kuwa imebaini yalipo mabaki yote ya ndege ya AirAsia namba
QZ8501.
Maafisa wameeleza kuwa umbo la kitu
kama ndege limebainika baada ya kutumia kipimo cha sonar scan katika
eneo ambalo zoezi la kuitafuta ndege hiyo katika bahari ya Java
linaendelea.
Maafisa hao wanamatumaini sanduku la
"black box" linalorekodi mawasiliano na taarifa nyingine za
ndege litakuwepo karibu na umbo lililobainika karibu na eneo ambalo
mkia wa ndege hiyo ulipatikana.
Ndege hiyo ilitoweka na kupoteza
mawasiliano ikiwa na abiria 162, ikitokea Surabaya nchini Indonesia
kwenda Desemba 28 kutokana na hali mbaya ya hewa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni