Mchezaji wa Wolfsburg, Junior
Malanda (20) amefariki dunia kwa ajali ya gari nchini Ujerumani.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya
Ubelgiji ya umri chini ya miaka 21, amecheza michezo 15 katika ligi
kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga katika msimu huu, pamoja na
mmoja wa Ligi ya Uropa dhidi Everton.
Mkurugenzi wa Wolfsburg Klaus Allofs
amesema katika taarifa yake kwa umma, kuwa wameshtushwa mno na kifo
cha mchezaji huyo, na wanashindwa hata kuamini kama ni kweli Malanda
ameaga dunia.
Malanda kulia wakati wa uhai wakifanya vitu vyake uwanjani


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni