Kijana mmoja mwenye asili ya Mali
ambaye ni Muislam amepongezwa kuwa ni shujaa, baada ya kuwaficha
wateja kwenye jokofu katika duka la Wayahudi, Jijini Paris ambalo
lilivamiwa na mtu mwenye silaha katika moja ya matukio ya ugaidi
nchini Ufaransa.
Raia huyo Lassana Bathily, 24,
ambaye mfanyakazi katika duka hilo, aliwaongoza wateja waliojawa na
hofu katika majokofu makubwa ya duka hilo la Hyper Cacher lililopo
Porte de Vincennes, Jijini Paris.
Tangu kufanya tukio hilo la kufikiri
haraka kuzima majokofu hayo na kuwaingiza wateja 15 na kuwanusuru na
kifo kutoka kwa mtu mwenye silaha Amedy Coulibaly ambaye aliuwawa
baadae, Bathily amekuwa akipokea pongezi nyingi.
Polisi wakivamia duka Hyper Cacher kuwaokoa mateka
Watu waliookolewa wakitoa huku wakiangua vilio kwa hofu



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni