Zaidi ya watu 50 wamekufa na wengine
zaidi kujeruhiwa baada ya basi kugongana na lori la mafuta katika mji
wa Karachi nchini Pakistani.
Lori hilo la mafuta linadaiwa kuwa
lilikuwa katika mwendo kasi na likiendeshwa upande ambao si wake
wakati lilipogongana na bus hilo uso kwa uso na kisha magari hayo
yote mawili kulipuka moto.
Baadhi ya abiria wa basi ambao
walikuwa juu ya basi hilo, waliweza kuruka na kunusuru maisha yao,
lakini wengi wa abiria waliokuwa ndani ya basi walishindwa kujinusuru
na kuungua moto. Dereva wa lori hilo inadaiwa alikimbia baada ya
kusababisha ajali hiyo.
Miili ya watu iliyoungua ikiwa kwenye mifuko kwenye chumba cha kuhifadhia maiti


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni