Viongozi wa dunia wamekusanyika
Jijini Paris katika kuelekea kuanza maandamano makubwa katika Jiji
hilo kuu la Ufaransa kwa ajili ya kuonyesha mshikamano, ikiwa ni siku
tatu tu kupita tangu kutokea matukio ya ugaidi yaliyouwa watu 17.
Baadhi ya viongozi wakuu 40
watahudhuria maandamano hayo, ambayo yanatarajiwa kuyazidi kwa idadi
ya watu maandamano ya jana yaliyohudhuriwa na watu laki 7.
Maafisa polisi wapatao 2,000 na
wanajeshi 1,350 wamesambazwa katika Jiji la Ufaransa kulianda usalama
wa waandamanaji.
Mashada ya maua yakiwekwa kuomboleza vifo vya watu 17 jijini Paris



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni