Maelfu ya wanakijiji wamekimbia
nyumba zao eneo Kashmir linalotawaliwa na India wakati vikosi vya
India na Pakistani vikipambana kwa silaha katika jimbo la hilo.
Karibu wanajeshi 10 wa India na
Pakistani na raia wameuwawa katika kipindi cha wiki moja iliyopita ya
vita.
Nchi zote mbili zimekuwa zikitupiana
lawama kwa kuanzisha mapigano hayo. Makubaliano ya kusitisha mapigano
ya mwaka 2003 bado yanaendelea lakini majirani hao wamekuwa
wakishutumiana kwa kuyakiuka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni