Chama cha Taifa cha Wazazi nchini
Kenya kimeitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya walimu
waliogoma, na kusema wanakaidi amri ya mahakama inayowataka kusitisha
mgomo wao huo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Bw.
Nathan Barasa, ametahadharisha kuwa uwezo wa mahakama utadharauliwa
iwapo walimu wanaoendelea kukaidi amri ya mahakama hawatoadhibiwa,
kwa ukaidi.
Aidha, Bw. Barasa amesema vyama vya
walimu nchini Kenya ni kama vimewafanya mateka wazazi na wanafunzi,
kutokana na kutumia visivyo mamlaka waliyonayo kwa walimu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni