Makamu wa rais wa Fifa Prince Ali
Bin Hussein atachuana na rais wa sasa Sepp Blatter kuwania uongozi wa
shirikisho hilo la soka duniani.
Mwana huyo wa Familia ya Kifalme ya
Jordan, Prince, 39, atasimama kugombea urais wa Fifa katika
uchaguzi utakaofanyika Mei 29 mwaka huu, ambapo Blatter pia atawania
muhula wa tano.
Prince Ali amesema huu ni wakati wa
kubadilisha utawala wenye utata, na kurejea kwenye njia ya mchezo wa
soka.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni