Mahakama Kuu ya Kenya leo imesitisha
kwa muda utekelezaji wa baadhi ya vifungu vya sheria yenye utata ya
usalama, wakati ikingojea usikilizaji wa kesi ya msingi
iliyofunguliwa na muungano wa Cord kuipinga sheria hiyo.
Miongoni mwa vifungu vya sheria
vilivyositishwa kutumika ni pamoja na kifungu namba 12, 29, 48, 56,
58, na 58. Katika uamuzi wake Jaji Justice George Odunga amesema
baadhi ya vifungu vinakiuka haki za msingi.
Kiongozi wa muungano wa Cord Raila
Odinga amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Mahakama Kuu, na kusema
kupitia mahakama imeweza kulinda haki za watu.
Kiongozi wa Cord Bw. Raila Odinga kati kati akinyanyua mkono juu kufurahia uamuzi wa mahakama


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni