Zoezi la kuitafuta chini ya bahari
ndege ya AirAsia namba QZ8510 ambayo ilianguka baharini siku ya
jumapili, linatarajia kuanza baada ya kuwasili kwa vifaa maalum vya
uzamiaji.
Timu ya waupelelezi ya Ufaransa
itatumia vifaa maalum vyenyeuwezo mkubwa wa kubaini kitu majini
katika kujaribu kutafuta kifaa cha ndege cha kurekodi takwimu cha
black box.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200
iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya, Indonesia kwenda Singapore
ilitoweka ikiwa na watu 162. Hakuna mtu aliyebainika kuwa hai hadi
sasa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni