Kanye West ameuanza mwaka mpya wa
2015 kwa kuachia wimbo mpya wa “Only One” alioshirikiana na Paul
McCartney.
Wimbo huo aliouimba kwa hisia kali
maalum kwa marehemu mama yake Donda West, umekuwa ukimtoa machozi mke
wake Kim Kardashian kila anapousikiliza.
Kwa mujibu wa Kim katika wimbo huo
ni kama Kanye West anatumika kutoa ujumbe wa Mama yake kwenda kwa
mtoto wao North West.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni