.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Januari 2015

MIILI MINGINE MINNE YAPATIKANA BAHARINI KATIKA MSAKO WA NDEGE YA AIRASIA

Miili minne zaidi ya watu imepatikana katika bahari ya Java wakati wa zoezi la kutafuta mabaki ya ndege ya AirAsia namba QZ8501 likiingia wiki ya pili.

Mkuu wa timu inayoendesha zoezi la kuitafuta ndege hiyo Bambang Soelistyo amesema hadi sasa miili 34 imepatikana ikiwemo na mabaki matano ya vipande vya ndege hiyo.

Hata hivyo hali mbaya ya hewa imewalazimisha wazamiaji kusitisha jaribio la kuifikia ndege hiyo kwenye eneo la chini ya bahari ambapo miili mingi ya watu inaaminika imekwama. Ndege hiyo ilianguka ikiwa na abiria 162.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni