.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Januari 2015

MTOTO MWENYE ASILI YA ROMA ANYIMWA ENEO LA KUZIKIWA NA MEYA WA UFARANSA

Mtoto mchanga wa kike mwenye asili ya Roma, amenyimwa eneo la kuzikiwa na meya mmoja nchini Ufaransa, na kupelekea kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa kundi la wanaharakati wa haki za binadamu.

Mtoto huyo aliyefariki dunia siku ya Krismasi, kwa kifo kilichotokana na maradhi yanayowaandama watoto wachanga, amenyimwa eneo la kuzikwa huko Champlan, kusini mwa Jiji la Paris.

Meya wa Champlan amesema kipaumbele cha eneo la kuzikia anatoa kwa walipa kodi tu, hata hivyo Meya wa eneo la jirani la Wissous, Richard Trinquier amekubali kutoa eneo la kumzika mtoto huyo na kusema uamuzi wa meya mwenzake ni wa ajabu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni