Korea Kaskazini imeelezea vikwazo
vipya ilivyowekewa kutokana na kushambulia wavuti ya kampuni ya
filamu ya Sony, kuwa havina sababu yoyote na ni sera za uhasama za
Marekani.
Marekani imeziwekea vikwazo taasisi
za Korea Kaskazini pamoja na watu binafsi 10, baada ya Shirika lake
la Ujasusi la FBI, kuilaumu serikali ya Pyongyang kwa kushambulia
wavuti ya Sony.
Korea Kaskazini imekanusha kuhusika
na tukio hilo, hata hivyo ilipongeza kitendo hicho cha kushambuliwa
kampuni ya Sony.
Tukio hilo lilitokea wakati kampuni
Sony ikiwa inakaribia kutoa filamu ya The Interview, ambayo inaelezea
jaribio la kutaka kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni