Zoezi la kutafuta mabaki ya ndege ya
AirAsia namba QZ8501 katika bahari ya Java linaingia katika wiki ya
pili, huku hali mbaya ya hewa ikikwamisha operesheni hiyo.
Wazamiaji wanatarajia kubadilikka
kwa hali ya hewa na kuwa nzuri, hata hivyo bado wanalazimika kuchukua
tahadhari kwa sasa.
Kitu kikubwa cha tano kinachozaniwa
kuwa ni mabaki ya ndege hiyo, kimeonekana chini ya bahari, na mwili
mmoja umepatikana na kufanya idadi ya miili iliyopatikana kufikia 31.
Ndege hiyo ilianguka baharini
ikitokea Surabaya nchini Indonesia kwenda Singapore jumapili ya wiki
iliyopita ikiwa na watu 162.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni