Mtu mwenye silaha amemuua polisi
mwanamke leo Jijini Paris, siku moja tu kupita tangu vijana wawili
wanaharakati wa Kiislam kuwauwa watu 12 katika ofisi za jarida moja
nchini Ufaransa.
Mtu mwingine amejeruhiwa vibaya
kwenye shambulio hilo katika kitongoji cha kusini mwa Montrouge,
ambapo aliyetekeleza shambulio hilo alitoroka.
Haikufahamika mara moja iwapo tukio
hilo linauhusiano na la kwenye ofisi za jarida la Charlie Heddo
yalipotokea mauaji jana, na kuitia hofu Ufaransa.
Polisi inawashikilia watu saba,
ikiendelea kuwasaka ndugu wawili waliohusika katika tukio la jana,
huku mtu mmoja wa tatu akijisalimisha.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni