.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Januari 2015

KIM KARDASHIAN NA MUMEWE KANYE WEST WAPITISHWA MLANGO WA KAWAIDA NA KUKAGULIWA KAMA ABIRIA WENGINE

Hakuna staa wala huduma maalum hapa!!: Mwanadada Kim Kardashin akikaguliwa na mmoja wa maofisa wa uwanja wa ndege wa LAX nchini Marekani jumatano usiku kabla ya kuendelea na safari akiwa ameaongozana na mumewe mwanamuziki Kanye West. Wengi walitaraji mastaa hao wengepitishwa sehemu maalum ( VIP ) tofauti na abiria wengine.
Jamani hunijui, mimi ndio Kim mke wa Kanye West: Ni kama anauliza Kim Kardashian nyota wa kipindi cha luninga cha Keeping Up With The Kardashian wakati akiendelea kukaguliwa uwanja wa ndege ili aendelee na safari yake.
Wewe tulia niendelee kukukagua, ustaa wako huko hapa kazi tu ili tuwe na uhakika wa usalama wa ndege zetu.
Kim Kardashian akiwa amevua viatu tayari kupita katika kifaa maalum cha ukaguzi. Aliyesimama katika kifaa hicho tayari kukaguliwa ni mumewe Kanye West.
Baada ya kukaguliwa na mabegi yao tayari kwa safari, huku Kanye West akiongea na mashabiki wake aliokutana nao uwanjani hapo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni