.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Januari 2015

MWILI WA MTOTO ALIYENYIMWA ENEO LA KUZIKWA NA MEYA KUZIKWA LEO UFARANSA

Mtoto mwenye asili ya Roma atazikwa kwenye makaburi Ufaransa baadae, huku kukiwa na mgogoro kuhusiana na taarifa za meya wa mji karibu na alipofariki mtoto huyo wa kike kugoma kutoa eneo la kuzikia.

Mtoto huyo atazikwa huko Wissous, kusini mwa Paris baada ya mji wa Champlan kuripotiwa kuinyima familia yake eneo la kumzika, hata hivyo meya wa mji huo jana alikanusha madai hayo baada ya kuibua shutuma za wananchi.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, amekiita kitendo hicho kuwa ni sawa na tusi kwa Ufaransa, na afisa wa nchi hiyo anayehusika na kulinda haki za binadamu ametangaza kuanza kwa uchuguzi wa tukio hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni