Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amefanya ziara ya kushtukiza katika mkoa wa Dar es salaam, ambapo katika ziara hiyo amefanikiwa kukamata wezi wa maji 12. Pia Mh Makalla awatimua mameneja wa maji wa Boko na kimara kutokana na utendaji wao mbovu. Katika ziara hiyo ya ghafla, Mh Mkalla ametangaza operasheni kubwa zaidi kusaka wezi wa maji. Hapa Naibu Waziri huyo wa Maji akiongea na wananchi wa Boko.
Mh Makalla akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojitokeza kutoa maoni yao wakati waziri huyo aipokuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya maji maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Hapa ilikuwa maeneo ya Manzese
Ziara imepamba moto kuhakikisha wananchi wa jiji wanapata maji na kuwakamata wanaohujumu miundombinu ya maji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni