Polisi nchini Ufaransa wamelizingira
jengo moja katika mji wa kaskazini, ambalo watu wawili wanaotuhumiwa
kuhusika mauaji katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo,
wanadaiwa kuwamo.
Milio ya risasi imesikika na watu
kadhaa inasemekana wamejeruhiwa katika eneo la Dammartin-en-Goele,
lililopo kilomita 35 kutoka Jiji la Paris.
Hatua hiyo imefikiwa ikiwa karibu
saa 48 kupita tangu kutokea shambulio katika ofisi za jarida la
vibonzo la Charlie Hebdo na kuuwa watu 12.
Polisi wakikimbilia kulizingira jengo hilo
Uangalizi hadi angani kuhakikisha hatoki mtu



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni