Mahakama ya Mombasa leo imekataa
kumuachia kwa dhamana mfanyabiashara mkubwa wa biashara haramu ya
meno ya tembo Feisal Mohammed Ali maarufu kwa jina la Feisal Shahbal.
Mfanyabiashara huyo alikamatwa mwezi
uliopita na Interpol nchini Tanzania kwa tuhuma za kufanyabiashara
kusafirisha meneo ya tembo kilo 2,152 yenye thamani ya shilingi
milioni 44 za Kenya.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Justus
Kituku amekataa ombi la dhamana kwa madai kuwa kunauwezekano
mtuhumiwa Feisal Mohammed Ali asirudi kusikiliza kesi yake baada ya
kupewa dhamana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni