.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 26 Januari 2015

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI KWA ZIARA YA KIKAZI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed,Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

                                                                                                         PICHA NA IKULU

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni