
Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makala mwenye shati maua akicheza ngoma wakati akipokelewa kijiji cha Manza wilayani Mvomero.
Mh Makalla amepokelewa kwa shangwe na wananchi wa jimbo lake ambapo wamemtaka agombee tena ubunge katika uchaguzi ujao. Wananchi hao hawakusita kusifia utendaji wake mzuri, mchapakazi, mkweli na amefika vijiji vyote 130 jimboni kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Katika ziara hiyo, Mh Makalla alishiriki chakula na walemavu katika kijiji cha Chohero na kuwakabidhi mbuzi kumi wa maziwa na nyama, pia alizindua na kukichangia kikundi cha kikoba cha faidika kijiji cha Manza, alisimamia uchimbaji wa kisima kijiji cha Kimambila-Mzumbe.
Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, Mh Amos Makalla akikabidhi kikundi cha Faidika kijiji cha Manza mchango wa shilingi laki tano tasilimu.
Mbunge wa jimbo la Mvomero ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akikabidhi mbuzi kumi kwa ajili ya walemavu kumi waa kijiji cha Chohero- Mvomero.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni