Mshambuliaji Fernando Torres
amerejea Atletico Madrid na kuanza kwa ushindi dhidi ya Real Madrid
wa mabao 2-0 katika mzunguko wa kwanza wa 16 bora katika Kombe la
Copa del Rey.
Umati wa mashabiki 46,800 walikuwapo
kumshuhudia mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea akirejea
katika klabu hiyo ya Atletico Madrid ambayo ndiyo aliyoanzia
kung'ara.
Magoli ya Atletico Madrid yalifungwa
na Raul Garcia kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu, ambapo
Jose Maria Gimenez alitumbukiza la pili kwa mpira wa kichwa.
Torres na Raul Garcia wakishangilia goli
Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wakishika viuno hoi kwa kipigo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni