Polisi nchini Ufaransa wamewataja
ndugu wawili kuwa ni watuhumiwa wa tukio la shambulio lililofanywa
katika ofisi ya jarida la Charlie Hebdo, wakati msako ukiendelea.
Polisi wametoa picha za ndugu hao
Cherif na Said Kouachi, na kuwaelezea kuwa ni watu hatari wenye
silaha na kutoa hati ya kukakamtwa kwao. Mtuhumiwa watatu
amejisalimisha mwenyewe.
Nchi ya Ufaransa imetangaza siku
moja ya maombolezo ya vifo vya wanahabari hao 12 waliouwawa katika
shambulio hilo.
Shambulio hilo limelaaniwa na
viongozi wa dunia, huku rais Barack Obama akisema yupo tayari
kuisaidia Ufaransa kuwasaka wahusika wa tukio hilo.
Polisi wakiweka ulinzi katika sehemu ya tukio
Maombolezo yakiendelea nchini Ufaransa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni