.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 27 Februari 2015

KUMEKUCHA NSSF REAL MADRID SPORTS ACADEMY


Baada ya uandikishaji kwa ajili ya kufuzu kujiunga na NSSF Real Madrid Sports Academy, awamu inayofuata ni ya majaribio ambayo itafanyika Jumamosi tarehe 28 Februari 2015 kwenye viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:45 asubuhi. 

Majina ya vijana watakao hudhulia awamu hii yamechapishwa kwenye magazeti ya Mwananchi, Majira na Mtanzania leo tarehe 27 Februari 2015.

Majina ya vijana watakao hudhulia majaribio ya awamu nyingine yatachapishwa kwenye magazeti ya wiki ijayo.

Kwa wale walio orodheshwa wanaombwa kufika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza majaribio.

Pia wazazi au walezi wanaombwa waambatane na watoto wao wakiwa wamewapatia vifaa vya michezo kama vile viatu,soksi, Shin guard, kaptula na flana ya michezo, maji na gharama za usafiri wajitegemee.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni