Vikosi vya jeshi la Kenya
vitaendelea kuwepo nchini Somalia kwa mwaka mmoja zaidi baada ya
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Raychelle
Omamo, amesema wameupokea uamuzi wa kuendelea kuwa sehemu ya vikosi
vya Umoja wa Afrika nchini Somalia na kutoa wito wa kutaka msaada
zaidi wa kukabiliana na ugaidi.
Vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Kenya,
vimekuwa vikisiadia kuikomboa Somalia ambayo imekuwa ikikabiliwa na
mashambulio ya wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni