Mshambuliaji mahiri wa Real Madrid, Cristaiano Ronaldo akiruka juu na kupiga kichwa mpira uliokwenda moja kwa moja golini na kumuacha mlinda mlango wa Schalke, Timon Wellenreuther akiwa hana la kufanya.
Mabao mawili ya katika kila kipindi yalitosha kuwapa ushindi wa mabao 2-0 Real Madrid dhidi ya wenyeji wao Schalke katika mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Alikuwa Cristiano Ronaldo aliyetangulia kufunga bao la kwanza katika dakika ya 25 kabla ya Marcelo hajafunga bao la pili katika dakika ya 78 ya kipindi cha pili na kuwanyamazisha kabisa mashabiki wa Schalke waliokuwa wamefurika uwanjani kuishangilia timu yao.
Mchezaji wa Real Madrid, Marcelo akifurahia na kocha wake Carlo Ancelotti baada ya kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Schlake.
Mashabiki wa Schalke wakiwa wamefurika kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao iliyojikuta ikitandikwa mabao 2-0 na wageni wao Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Unaona kule weweeeee!!! ile sio sawa hata kidogo. Kocha mkuu wa Real Madrid Ancelotti akilalamika jambo kwa mwamuzi msaidi wakati timu yake.ilipokuwa ikicheza na Schalke
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni