.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Februari 2015

MISRI YATOA WITO WA KUTAKA KUWEPO USHIRIKIANO KUPAMBANA NA IS LIBYA

Misri imetoa wito wa kutaka kuwepo ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na wapiganaji wa kundi la dola ya Kiislam IS nchini Libya.

Rais Abdel Fattah al-Sisi amesema kinachofanyika nchini Libya ni tisho kwa amani ya dunia na usalama.

Kauli ya rais al-Sis imekuja wakati ndege za kivita za Misri zikishambulia maeneo ya wapiganaji wa IS katika kujibu mapigo kwa tukio la kuuwawa kwa kuchinjwa Wamisri 21 wakristo na wapiganaji wa IS.

Nchi ya Libya imekuwa katika machafuko tangu mwaka 2011, huku kukiwa na vikundi vya wapiganaji vipatavyo 1,400 vikipigana kushika utawala wa maeneo, licha ya kuwa pia na serikali mbili kinzani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni