Mwakilishi wa jimbo la Magomeni (CCM ) na mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Salmin Awadh Salmin (kushoto) enzi za uhai wake akizungumza na mjumbe wa baraza hilo Ali Mzee Ali (kuteuliwa na Rais) wakati wa kikao cha baraza huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Maktaba.
Mwakilishi wa jimbo la Magomeni kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Salmin Awadh Salmin amefariki dunia ghafla mchana huu huko visiwani Zanzibar.
Taarifa toka visiwani humo zinasema kuwa, Mheshimiwa Salmin Awadh ambaye pia alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, amefariki dunia wakati akishiriki kikao cha CCM kilichokuwa kinafanyika katika ofisi kuu ya chama hicho Kisiwandui.
Alithibitishwa na daktari kuwa amefariki dunia mara baada ya kufikishwa hospitali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni