Rapa nyota aliyetamba katika miaka
ya nyuma Vanilla Ice amefunguliwa mashtaka yahusuyo wizi huko
Lantana, Fla, karibu na mahali anapojenga nyumba kwa ajili ya shoo
yake ya uhalisia iitwayo “The Vanilla Ice Project,”.
Ice ambaye jina lake halisi Robert
Van Winkle alishikiliwa na polisi jana na kufunguliwa shtaka la wizi
uliotokea mwezi uliopita. Mkuu wa kituo cha polisi cha Lantana Sean
Scheller amesema katika wizi huo vitu vikubwa vikiwemo hita ya bawa
la kuogelea, baiskeli na vitu vingine viliibiwa.
Baada ya kufanya uchunguzi polisi wa
Lantana walifanya uchunguzi kwenye nyumba ya jirani ya ile ambayo
Vanilla Ice anaifanyia ukarabati na kukuta baadhi ya vitu
vilivyoibiwa kwenye nyumba ya Ice na kuvirejesha kwa mwenyewe.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni