.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 14 Februari 2015

NAIBU WAZIRI WA MAJI, MH AMOS MAKALLA AKAGUA MIRADI YA MAJI KIJIJI CHA EMBURUKOI NA KANDASHI WILAYANI SIHA MKOANI KILIMANJARO


Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makalla ameendelea na ziara yake na leo ametembelea wilaya ya Siha kwa kuongea na viongozi wa wilaya ya Siha, kutembelea miradi ya maji kijiji cha Emburukoi, Kijiji cha Kandashi na bodi za maji za Lawale Fuka na Magadini Makiwarau.
 
Amezipongeza bodi za maji za Lawate Fuka na Magadini Makiwarau kwa kujiendesha vizuri na kutoa huduma kwa ubora wa hali ya juu kwa wananchi zaidi ya 100,000
 
Aidha amezitaka bodi za maji za daraja C na kamati za maji kufika wilaya ya Siha kujifunza
 
Kuhusu mradi wa kutoa maji mto simba kupeleka Longido ameagiza viongozi wa wilaya ya Siha na Longido, watalaamu wa bonde la kati na Pangani na ofisi ya katibu Tawala mkoa wa Arusha kuwa na vikao vya ujirani mwema wakati huu ambao wizara ya maji inatafuta fedha za kutekeleza mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akisalimiana na viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Siha.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akiangalia kituo cha kuchotea maji Sanya Juu.Naibu Waziri Maji,Mh Amos Makalla akipata maelezo mradi wa maji kijiji cha Kandashi toka kwa mhandisi maji wilaya injinia Christine Kessy.
Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla akikagua ujenzi wa tanki kijiji cha Embukoi.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni