Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa elimu na ufundi Kassim Majaliwa
wakiangalia jaribio la Sayansi lililokuwa likifanywa na mwanafunzi katika shule
ya sekondari ya kata ya Majani ya Chai huko Kipawa jijini Dar es Salaam.Awali
Rais Kikwete alizindua maabara za sayansi katika shule hiyo na baadaye
alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Sera ya Elimu na
Mafunzo ya mwaka 2014 katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari
Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Bwana Said Meck Sadik.
(Picha na Freddy Maro)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni