.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Februari 2015

PAPA FRANCIS ALAANI MAUAJI YA WAKRISTO 21 RAIA WA MISRI

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amelaani kuuwawa kwa kuchinjwa wakristo 21 wa dhehebu la Coptic raia wa Misri, na wapiganaji wa kundi la dola ya Kiislam IS nchini Libya, na kutangaza kuwa waliouwawa ni mashahidi wa imani na kusema kuwa wakristo wote ni wamoja bila ya kujali madhehebu yao.

Papa amelazimika kutoa kauli yake katika mkutano usio rasmi baada ya vyombo vya habari vya nchini Libya kutoa taarifa za kutekwa Wamisri wengine 35 katika eneo moja la Libya linaloshikiliwa na wapiganaji wa kundi la IS.

Utekaji nyara huo wa raia wengine wa Misri umekuja baada ya Misri kujibu mapigo ya dola ya Kiislam IS kwa kufanya mashambulizi ya anga katika kambi zao, ambapo mkuu wa jeshi la nchi hiyo amesema watu 50 wameuwawa.
                     Wapiganaji wa IS wakijiandaa kuwachinja Wakristo 21 raia wa Misri 
                            Bahari ya ikiwa imetapakaa damu ya watu 21 waliouwawa kikatili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni