.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Februari 2015

VIKOSI VYA NIGERIA VYATWAA MIJI MIWILI ILIYOKUWA IKISHIKILIWA NA BOKO HARAM

Vikosi vya jeshi la Nigeria vikisaidiwa na mashambulizi ya angani vimetwaa miji miwili ya Monguno na Marte iliyokuwa ikishikiliwa na kundi la Boko Haram.

Wakati huo huo nchi ya Cameroon imesema jeshi lake limewauwa zaidi ya wapiganaji 80 Boko Haram na kuwakamata watu 1,000 wanaowaunga mkono.

Vile vile nchi Niger nayo jana imesema imewakamata watu 160 wenye uhusiano na kundi la Boko Haram tangu Februari 6, mwaka huu.

Nchi za Nigeria, Chad, Cameroon pamoja na Niger hivi karibuni zimeunda ushirikiano wa kijeshi dhidi ya kundi hilo la wapiganaji wa Kiislam.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni